Jumapili Sept 9, 2012 ulifanyika uzinduzi rasmi wa video iliyofanywa jiji la Joz South Africa ya wimbo wa Baadae wa Ommy Dimpoz pale Maisha club. Video ilisubiriwa kwa hamu sana kiasi ambacho hata baadhi ya Tv stations zilikuwa zikiitumia ile Teaser ya making iliyotolewa takribani wiki mbili zilizopita.
Haya sasa video hiyo imeanza kuonekana katika vituo vya runinga hapa bongo, je imekata kiu uliyokuwa nayo mara baada ya kuona ile teaser ya making yake? Itazame video yote hapo chini