Muimbaji mrembo kutoka nchini Colombia anayesifika kwa kushake kiuno chake ipasavyo, Shakira, amethibitisha kupitia blog yake kuwa yeye na mpenzi wake mcheza soka wa timu ya Barcelona, Gerard Pique wanatarajia kupata mtoto na hivyo atakipumzisha kidogo kiuno hicho.
Aliandika: “Kama baadhi yenu mnavyofahamu Gerard na mimi tunafurahia ujio wa mtoto wetu wa kwanza! Katika muda huu tumeamua kuupa kipaumbele muda huu maishani mwetu na kuachana na shughuli za promotion zilizopangwa siku sijazo.”
“Hii inamaanisha kuwa sitaweza kuwa sehemu ya tamasha la muziki la iHeartRadio … Ningependa kuishukuru Clear Channel na mashabiki wangu kwa upendo wao usiokoma na uelewa wao. Big kiss!” aliongeza.
Kwa mujibu wa jarida moja la nchini Colombia mtoto wao anatarajiwa kuzaliwa January mwakani.
Limeongeza kuwa wapenzi hao tayari wameshampa jina la utani mtoto wao huyo ajaye la Ulicito.