|
sir chande |
Umechoka kusikia habari za Ufreemason? Tunaamini jibu ni ndio. Lakini hebu chukua muda kufahamu ukweli kiduchu tu kutoka kwa kiongozi mstaafu wa jamii hiyo nchini Tanzania, Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Sir Andy Chande ili uanapo vichwa vya habari vya magazeti ya udaku vinavyowaita baadhi ya wasanii wa Bongo Flava mafreemason (kutokana na kununua gari za milioni 70 wakati hata wakulima wa kahawa mkoani Kagera wanaweza kumudu kununua), na uweze kuwaelimisha kidogo wanaoamini hivyo.
Kwa mujibu wa Sir Andy, ukiwa mwanachama wa Freemason hakuna kipato ama ongezeko la fedha lolote unalolipata. “There is no financial benefits, no no,” alisisitiza Sir Andy kwenye kipindi cha The Interview cha Clouds TV kilichoruka jana usiku.
Hiyo ndio ilikuwa ni pointi ya msingi kuifahamu kwakuwa watanzania wengi wameaminishwa kuwa baadhi ya watu wametajirika baada ya kujiunga na ufreemason, kitu ambacho kwa mujibu wa Sir Chande si kweli hata kidogo.
Katika kipindi hicho mzee huyo amesimulia mengi ya ndani kuhusiana na freemasonry na kuongeza kuwa hakuna kitu cha siri kwenye jamii hiyo. “Hakuna kitu ambacho hujakisikia, ni kinyume kabisa ya mengi uliyokuwa ukiyasikia, kumbe mwisho wa siku kama alivyoelezea Mzee Chande, freemasonry ni kuhusiana na upendo, urafiki na ukarimu zaidi na kuitakia jamii mema na mambo ya aina hiyo,” alifafanua mtangazaji wa kipindi hicho, Gerald Hando.