Baada ya kuonyesha uwezo kwenye tasnia komedi nchini, Msanii maarufu wa vichekesho kutoka kundi la Orijino Komedi kwa jina la Wakuvwanga ameamua kubadili fani na kuamua kujitosa kwenye fani ya muziki. Msanii huyo amekamilisha albam yenye nyimbo tisa na kutengeneza video zake katika albamu alioipa jina la “Kato“.
Alitaja baadhi ya nyimbo katika albamu hiyo kuwa ni Angwisa, Ndoa, Anacheza, Analia na Viatu sio watu. Akiongea mwishoni mwa wiki Wakuvwanga aliwataka mashabiki wake waipokee albamu hiyo pindi itapokuwa sokoni.
Kutokana na Wakuvwanga kuingia kwenye fani ya Muziki amefanya idadi ya wasaniii wa kundi ilo kuongezeka baada ya wasanii wenzake watatu wa kundi hilo Joti, Mpoki kufanya muziki kwa sasa, bila kumsahau Masanja ambaye anaimba nyimbo za Injili.