Matunda ya kushiriki Big Brother Africa yameanza kuiva kwa msanii wa kike wa Nigeria aliyeiwakilisha nchi hiyo mwaka huu, Goldie.
Hiyo ni baada ya kuanza kupiga collabo na wasanii mbalimbali wa Afrika akianza na Navio wa Uganda.
Leo kupitia Facebook, Navio amepost picha aliyopiga na mrembo huyo huku akiandika, “In the studio with my home girl @GoldieHarvey from BBA. Kilt it in studio! 2012 is about get realer!”
Hivi karibuni Goldie alikuwa nchini Kenya ambako alikutana na Prezzo japo haijulikani kama alifanya collabo na msanii yeyote wa huko.
Kwakuwa Kenya na Uganda amekwishazitembelea, tunasubiri tuone kama atafikiria pia kuja Bongo!!