HII NDIO SABABU LIL WAYNE ANAFANANISHWA NA ELVIS PRESLEY.
Saturday, September 22, 2012
Lil
wayne ameingizwa kwenye rekodi ya wasanii wenye nyimbo nyingi
zilizoingia kwenye chart za muziki za dunia `Bilboard Hot 100' baada ya
wimbo alioshirikishwa na Juciy J `Bandz A Make Her Dance' ft Lil Wayne
na 2 Chainz kuingia kwenye chart hio na kushika namba 71. Hii
inahesabika kama mara ya 108 kwa Lil Wayne kuwepo na wimbo kwenye chart
hio sawa na mfalme wa Pop Elvis Presley.Hizi ni takwimu za wasanii wa
kiume wenye nyimbo nyingi zaidi kwenye chart za Bilboard Hot 100.
Kupitia
hizi nyimbo 108 ,Lil wayne ana nyimbo zake mwenyewe 42 na zingine alizo
shirikishwa 66. Nyimbo zake mbili zilifika namba 1, ambazo ni “
Lollipop ” and “ Down “. Wimbo mpya wa Lil Wayne “ No Worries “
aliomshirikisha Detail upo namba 58 na unapanda zaidi . Haya nimafanikio
makubwa kwa Lil wayne na anahitaji wimbo mmoja tu kwenye chart hizo
ilikufunika rekodi ya Elvis Presley.
Tags:
Uncategorised