Proscovia Alengot Oromait: Msichana mwenye miaka 19 aliyeshinda ubunge!!
Saturday, September 22, 2012
Proscovia Alengot Oromait wa nchini Uganda ameweka rekodi barani Afrika kwakuwa mbunge mwenye umri mdogo kuliko wote kwa kuingia mjengoni akiwa na miaka 19 tu.
Kama unadhani aliupata kwa viti maalum, futa wazo hilo kwakuwa msichana huyo ameshinda kwenye uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge kilichokuwa kikikaliwa na baba yake.
Awali Oromait alikuwa amepanga kwenda chuo lakini aliamua kuingia kwenye siasa baada ya kifo cha baba yake Michael Oromait mwezi July, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Usuk lililopo mashariki mwa Uganda.
Akiwa na miaka hiyo, Oromait aliwagalagaza wagombea watu wazima wanane ambapo alimzidi kura mara mbili mgombea aliyekuwa nyuma yake.
Shirika la habari la Associated Press limedai kuwa kuchaguliwa kwake kuna faida kwa chama tawala cha rais Yoweri Museveni.
Oromait amekuwa mbunge wa pili mwenye umri mdogo duniani.