|
Marehemu daudi |
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa
chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa
Daud Mwangosi ameuwawa
katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha
Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo.
Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni
katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa
risasi .
Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa
eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma
kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka
katika ofisi yao.
Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa
kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey
Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya
kukamatwa kwa
mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia
kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi
huyo na askari mmoja waliaguka chini .
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa
afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya
Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia
maiti .
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari
na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano
ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na
mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.
Mwili wa Marehemu Daudi ukiwa chini baada ya kulipukiwa na
bomu
Gari la Chadema lililovunjwa kioo wakati wa vurugu.
Mwandishi David mwenye sweta la rangi ya udongo akipiga
picha nusu saa kabla ya kifo chake