|
ney | |
Mtu anayejiita mchungaji hivi karibuni amemtabiria kifo rapper Ney wa Mitego kwa kudai kuwa atafariki kwa kuchomwa na kisu au kupigwa risasi.
Ney amesema mchungaji huyo alimfuata nyumbani kwake na mpaka picha zake anazo.
“Nilimrekodi pia, alikuwa anaongea kwa confidence sana, lakini mimi sitishiki na wala siogopi, mimi namtegemea mwenyezi Mungu. Hiki ninachokifanya ni kipaji cha pekee na hawajui kwanini najiamini na siwezi kuacha kukifanya hiki,” Ney alikaririwa jana Jumamosi kwenye kipindi cha Tagz Weekly cha DTV.
Ney amesema mtu huyo alimwambia kuwa ameoneshwa na mwenyezi Mungu, kwamba yeye ni nabii na ni lazika amfikishie ujumbe huo.
“Mwanzo alifika home, aliwakuta wadogo zangu, mimi nikasema amekuja from nowhere siwezi
kuongea naye, alianza kuongea na madogo, akawaambia
anataka kuonana na Ney mwenyewe, nikawaambia mwambie aondoke.
Nikaona
haina haja kwanini nisionge naye, aliacha namba za simu, dogo akampigia
akarudi, kurudi ndio akaongea aliyokuwa anaongea.”
”Watanzania wajue kuwa wameanza kutokea watu ambao wanatabiri kifo
changu ila nawaambia mimi najua siku yangu ya kufa labda wao waendelee
kufanya harakati zao ili kunifelisha na hawawezi kunifelisha, mwenyezi
Mungu ndio anajua mimi nafanya nini na wapi ambapo ntaishia.”
“Nilishawaahidi watanzania kwamba huu ni muziki wangu na hii ndio
hip hop na hizi ndio harakati ambazo natakiwa kuzifanya,”aliongeza.
Pia amesema siku za hivi karibuni amekuwa akipokea meseji za vitisho kutoka kwa watu wanaomtishia kumuua.