|
ben pol |
|
Mwimbaji mahiri Bongo fleva
Ben pol amesema kwa namna yoyote ile,video ya wimbo wake wa
pete uliotoka wiki iliyopita lazima aifanye nje ya nchi.Pete ni wimbo wake wa kwanza kutoka kwenye label yake ya awali
M-LAB.Ben pol ameonekana kuifuata idea ya mwenzake,
Ommy Dimpos aliyesafiri hadi africa kusini kufanya video yake ya
baadae.'' south africa ni wazo tu lililokuja, kwa hiyo chochote tunaweza tukafikiria,lakini kimsingi video yangu haitashutiwa hapa'',ben pol aliiambia power jam ya
EAradio.Amesema video hiyo anaweza kufanya na Ogopa djs jijini Nairobi kenya ama adam juma ambaye watasafiri nae hadi africe kusini